Ujenzi wa jumba litakalotumika na wachuuzi katika soko kuu la Kongowea utakamilika katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mhandisi na msanifu majengo katika Idara ya nyumba na makao katika Serikali kuu Aidah Munano alisema kuwa maswala muhimu yanatekelezwa kwa sasa na jengo hilo litakamilika baada ya kipindi cha miezi mitatu kutoka sasa, na kuwa swala hilo limeidhinishwa na wanakandarasi wanalishughulikia.

Akizungumza wakati alipozuru soko hilo la Kongowea mjini Mombasa siku ya Jumamosi ili kukagua shughuli za ujenzi, Munano alisema kuwa jumba hilo litapanua shughuli za kibiashara na kuwawezesha Vijana wengi kuendeleza kibiashara.

Munano alisema kuwa sababu kuu ya kukagua ujenzi huo ni kufuatia ujenzi wa kiholela ambao umekuwa ukitekelezwa na wanakandarasi licha ya kulipwa mamilioni ya fedha.

"Tumeonelea kufika mahali hapa na kukagua shughuli ya ujenzi kwani wanakandarasi wengi kupenda kufuja fedha na kujenga majengo yasiokuwa na msingi dhabiti," alisema Aidah.

Jengo hilo iwapo litakamilika litawakimu zaidi ya wachuuzi 1,500 katika soko hilo la Kongowea.