Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa kijiji cha Amakara, wadi ya Nyansiongo, kaunti ya Nyamira, wana kila sababu yakutabasamu baada ya ujenzi wa darasa la mafunzo ya shule ya chekechea kutamatika.

Akizungumza siku ya Jumanne wakati wa kudadisi jengo hilo, mwakilishi wa wadi ya Nyansiongo Jackson Mogusu aliwaomba wazazi kuwasajili wanao kupata mafunzo ya mapema yatakayo wafaa.

"Nawaomba wazazi kuchukua jukumu lakuwasajili wanao kupata mafunzo ya mapema, yatakayo wafaa katika maisha yao ya usoni,” alisema Mogusu.

Mwakilishi huyo aliiomba serikali ya Kaunti ya Nyamira kuwaajiri walimu wa chekechea kwa haraka huku akiinyoshea kidole cha lawama bodi yakuajiri wafanyi kazi wa umma kwenye kaunti ya Nyamira kwa kuchukua muda mwingi kuwaajiri walimu hao.

Mogusu alisema kuwa vituo vya mafunzo yachekechea vitaimarisha viwango vya masomo kwenye kaunti ya Nyamira.

Kituo hicho kinachotarajiwa kuzinduliwa rasmi na gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama siku ya Jumatatu wiki ijayo kinatarajiwa kupeana huduma za masomo kwa watoto kutoka kwenye wadi ya Nyansiongo na vitongoji vyake.