Katibu wa ujenzi na maendeleo ya mijini Aidah Munano, amesema kuwa zaidi ya asimilia 90 ya ujenzi wa Soko la Kongowea umekamilika.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akihutubia wanahabari alipozuru soko hilo kukagua jengo jipya linalojengwa sokoni humo, Munano alisema kuwa ukarabati wa soko hilo utakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

Munano alisema kuwa serikali ya kitaifa inashirikiana na ile ya kaunti katika mradi huo.

“Serikali kuu inashirikiana kwa karibu na ile ya kaunti kwa vile kama sote tujuaavyo, masoko yako chini ya serikali za kaunti,” alisema Munano.

Haya yanajiri baada ya kuzuka tetesi kuwa serikali hizo mbili zilikuwa zikizozana kuhusu aliyesimamia mradi huo.

Wafanyibiashara zaidi ya 1500 wanatarajiwa kuhamia katika jengo hilo la kisasa ambalo liligharimu shilingi milioni 320.

Wafanyibashara hao wamepongeza mradi huo kwa kusema kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza msongamano katika soko hilo.