Serikali kupitia Wizara ya Usafiri imeanza rasmi zoezi la ukaguzi wa mipango ya ujenzi wa daraja la kivuko cha Likoni katika Kaunti ya Mombasa.
Mkuu wa Idara ya Usafiri katika Kaunti ya Mombasa Tawfiq Balala amesema kuwa tayari wizara hiyo imeshatuma maafiasa wa kukagua ramani ya eneo hilo, zoezi ambalo litakalomalizika mwezi wa saba, mwaka huu kwa awamu ya kwanza.
Hata hivyo, Balala alisema kuwa kiwango cha fedha kitakachogharamia ujenzi wa daraja hilo kitatolewa baada ya ukaguzi huo, huku ikikadiriwa kuwa serikali ya kaunti itapata wafadhili katika ujenzi wa daraja hilo.
Ujenzi wa daraja hilo la Likoni ukikamilika basi hakutakuwa na haja ya wakaazi wa eneo hilo kutumia huduma za ferry kwani usafiri utakuwa wa moja kwa moja katika pande zote mbili.