Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Seneta wa Kaunti ya Nakuru, James Mungai, ameitikia wito wa wakazi wa eneo la Ndabibi kwenye kaunti ndogo ya Gilgil, wa kukarabati barabara katika eneo hilo.

Akizungumza na wakazi siku ya Jumanne katika eneo hilo la Ndabibi, meneja kutoka ofisi ya seneta huyo, Joseph Omondi, kwa niaba ya seneta huyo aliwahakikisha wakazi hao kuwa barabara hizo zitakarabatiwa katika juhudi za kutoa huduma bora kwa wananchi.

Omondi alisema kuwa mipango hiyo ya ukarabati wa barabara itaendelezwa katika maeneo bunge 11 yaliyo chini ya Kaunti ya Nakuru.

“Wakazi wa Ndabibi walikuwa wakilalamika kwamba barabara zao si nzuri na sasa seneta ameitikia wito wao na ameleta tinga hii leo. Amesema tinga hizo hazitaondoka katika eneo la Ndabibi kama barabara zote za eneo hili hazijatengezwa. Amenunua mashine za kutengeza barabara kwa hivyo msiwe na wasiwasi,” alisema Omondi.

Mary Nduta, mkulima, alitoa ombi kwa seneta kuhakikisha kuwa barabara hizo zinakarabatiwa kwa kasi ili kuwezesha mazao yao kusafirishwa kwa njia rahisi.

Pia ameelezea wasiwasi wake kutokana na mvua kubwa ambayo ametaja kama changamoto kwao katika usafirishaji wa mazao hadi sokoni.

“Tungeomba tutengenezewe barabara hii ili iwe rahisi kwa mazao yetu kusafirishwa hadi sokoni kwani mvua inaponyesha barabara hii huharibika,” alisema Nduta.

Robert Ngugi, mfanyibiashara katika eneo hilo aliunga mkono matamshi ya Nduta.

“Seneta anafaa atushughulikie haswaa kwa upande wa barabara kwa kuwa tumekuwa tukipata taabu kwa muda mrefu. Namuomba atusaidie ili mazao yetu yaweze kufika sokoni kwa muda ufao.