Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wadi ya Elburgon katika kaunti ya Nakuru Florence Wambui amekashifu vikali jamii ambazo bado zinaendeleza ukeketaji.

 Akizungumza siku ya Jumamosi huko Elburgon, Wambui alisema ni jambo la kusikitisha kuwa mtoto wa kike anazidi kudhulumiwa. 

"Tuko katika karne mpya na mtoto wa kike anafaa kukumbatiwa na kila mmoja katika jamii. Hatufai kuendelea kushuhudia visa vya ukeketaji" Wambui alisema.

Wakati huo huo,ametoa wito kwa mahakama kuhakikisha kwamba inashughulikia kwa kasi kesi zinazohusiana na dhuluma dhidi ya mtoto wa kike.

 Vile vike MCAhuyo alitoa wito kwa wakuu wa shule kuhakikisha kwamba watoto wa kike wanapata elimu sawa na mtoto wa kiume.