Ukosefu wa ajira miongoni mwa wakaazi wa Likoni na Kisauni umetajwa kama sababu kuu inayochangia katika kuendelea kuchipuka kwa makundi haramu katika maeneo hayo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Jumatatu, Mkuu wa polisi katika eneo la Kisauni Richard Ngatia, alisema kuwa vijana wengi katika eneo hilo hukosa ajira na hatimaye kujitosa kwenye visa vya utovu wa usalama na hata wengine kuanza kutumia mihadarati.

Ngatia ameongeza kuwa vijana hao hutumia hali hiyo ya uhaba wa ajira katika eneo hilo kama fursa ya kufanya mambo ambayo yako kinyume na maaadili ya jamii, akitoa mfano wa kundi ambalo linahanagaisha wakaazi Kisauni la Wakali Kwanza.

Aidha, alisema kuwa wanachama wa kundi hilo ni vijana wadogo ambao wanapaswa kuwa shuleni wakisoma.

“Watakaopatikana wakijihusisha na vitendo vya kihalifu wataadhibiwa kwa mujibu kwa sheria,” alisema Ngatia.

Aidha, aliwaomba wale ambao wanajihusisha na vitendo hivyo kujisalimisha katika vituo vya usalama na kuasi tabia hiyo potovu.