Ukosefu wa lishe umetajwa kama changamoto kuu kwa wakulima wa maziwa humu nchini. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya New KCC Matu Wamae alisema kuwa swala hilo limechangia kupungua kwa viwango vya maziwa kutoka kwa wakulima.

Akizungumza Jumanne katika mkutano wa kuhamasisha wakulima huko Njoro, Wamae alisema kuwa swala hilo linashughukulikiwa ili suluhu ipatikane. 

"Ni vyema tutatue swala hili ili kuimarisha kilimo cha maziwa," alisema afisa huyo.

Wakati huo huo, Wamae aliwataka wakulima wa maziwa kukumbatia kilimo cha nyasi spesheli kwa ajili ya lishe ya mifugo wao, na kutoa wito pia kwa wizara ya kilimo nchini kushirikiana na wakulima pamoja na wahisani wengine ili kuimarisha kilimo cha maziwa. 

Aliongeza kuwa bunge lafaa kupasisha sheria mhimu za kuhakikisha ubora wa lishe ya mifugo wa maziwa maarufu kama 'hay'.

Mkutano huo uliwaleta pamoja wakulima kutoka kaunti zote 47

Picha: Ng'ombe wa maziwa wakinywa maji. Ukosefu wa lishe ndio pigo kwa kilimo cha maziwa, kulingana na Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya New KCC Matu Wamae.