Ukosefu wa pesa za kuanzisha biashara miongoni mwa vijana ndio changamoto kubwa inayolemaza juhudi zao za kujiendeleza kupitia miradi mbalimbali.
Haya ni kwa mjibu wa rais wa World chapter Parliament Kenya Chapter Kennedy Omulo, ambaye amesema vijana wengi hawana ufahamu kuhusu namna ya kupata pesa hizo huku wengine wao wakilalama kuhangaishwa wanapotaka pesa kutoka kwa hazina ya uwezo na ile ya kustawisha vijana.
Omulo amesisitiza umuhimu wa vijana kujitokeza na kutoa mchango wao kwenye maswala muhimu ya uongozi na maendeleo na kuhakikisha kuwa haki zao zinaheshimwa.
Ametoa wito kwa serikali za kaunti kuweka mikakati kuhusu namna watakavyoshirikiana kwa pamoja na vijana ili kutatua changamoto zinazowakumba vijana
“Vijana wengi hawana fedha za kuwasaidia kwanzish miradi itakayowawezesha kujikimu kimaisha. Fedha zinaotokana na hazina za vijana na serikali vle vle hawajaweza kuzipokea,” alisema Omulo.