Seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko ameonekana kuwa na umaarufu si Nairobi tu bali pia katika kaunti ya Nakuru na kuwashangaza wengi wa viongozi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ilidhihirika katika mkutano wa Afraha wikendi iliyopita pale umati ulipoanza kupiga kelele na kutaka seneta huyo aruhusiwe kuhutubia wageni na wananchi katika uwanja huo.

"Sonko.....Sonko....sonko,"czilisikika sauti za umati.

Waziri wa Kawi Charles Keter hakuwa na budi ila kuitikia wito wa wengi na kumpa fursa Seneta Sonko kuhutubia umati wa watu waliohudhuria hafla hiyo ya maombi iliyojaa mbwembwe za kila aina.

"Sisi tumeteseka sana na Naibu Rais katika maombi na hata wakati mmoja tumeshikwa katika uwanja wa ndege lakini hatukufa moyo nachatimaye haki imetendeka na tunashukuru Mungu,'' alisema Sonko.

Hatua hiyo imewaacha baadhi ya viongozi wa Nakuru wakijiuliza maswali hasa ikizingatiwa kwamba Sonko ni Kiongozi wa Kaunti ya Nairobi lakini sifa alimiminiwa katika Kaunti ya Nakuru.