Wabunge katika kaunti ya Nakuru wametakiwa kuunda sheria zitakazo wavutia wawekezaji kuja katika kaunti hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria alisema kuwa ukosefu wa sheria mwafaka kumechangia katika ukosefu wa wawekezaji wengi katika kaunti.

Akiongea mjini Nakuru leo asubuhi, Gikaria alisema kuwa tangu bunge la kaunti liundwe, hakuna hata sheria moja ya kuwavutia wawekezaji ambayo bunge hilo limepitisha.

Aliwataka wabunge wa bunge la kaunti kutafakari na kiubuka na mbinu za kuwavutia wawekezaji ili kuunda nafasi zaidi za kazi kwa vijana katika kaunti.

Alisema kuwa kaunti ya Nakuru ina raslimali nyingi sana lakini hazitakuwa na maana iwapo wabunge wa kaunti hawatatunga sheria mwafaka za kuwezesha utumizi wa raslimali hizo.

“Nakuru ina uwezo wa kuwavutia wawekezaji wengi sana lakini kama hakuna sheria za kuwavutia basi hizi raslimali zetu zitakosa maana,” alisema Gikari.

“Wawakilishi wadi wanafaa kutumia bunge la kaunti kuunda sheria za kuwatongoza wawekezaji kwani hata unapotongoza msichana ,usipotumia lugha tamu hautampata,” alisema Gikaria.

Gikaria aliwataka wabunge wa bunge la kaunti kukoma kutumia muda mwingi katika shuguli zisizo na maana na badala yake wazingatie yale waliyochaguliwa kufanya.

“Badala yao kuzunguka mjini wakifukuzana na biashara zao wanafaa kutumia muda huo kuwahudumia wapiga kura walio wachagua na hilo sitakoma kuwaambia,” aliongezea kusema.