Zaidi ya wakimbizi 13, 400 wamejitolea kurudi Somalia katika miezi 18 zilizopita kulingana na umoja wa mataifa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na rekodi hizo, ni ngumu kufikia lengo la kuwarudisha wakimbizi 50,000 mwaka huu na 65,000 mwaka ujao. Malengo hayo yaliwekwa kupitia mkataba wa pamoja kati ya serikali ya Kenya, Somalia na UNHCR, mwaka wa 2013.

Shughuli za kurudi Somalia zimetatizwa kutokana na hali mbaya ya barabara katika kaunti ya Garissa. Hii imelazimisha UN kutumia ndege kuwahamisha wakimbizi hao ambayo inatumia pesa zaidi ya sh2.5 milioni kwa kila ndege. Haya ni kulingana na msemaji wa shirika la UNHCR, Andrew Neethan.

Zaidi ya wakimbizi elfu mia tatu arobanne, wengi wao kutoka Somalia, walibaki Daadab kufikia mwisho wa Aprili 2016, huku laki moja na elfu tisini kutoka Sudan Kusini wakihesabiwa katika kambi ya Kakuma kufikia mwezi Machi.

Kufuatia visa vya ongezeko la mashambulizi ya Al-Shabaab nchini, serikali ya Kenya ilifikia uamuzi wa kufunga kambi hiyo mwezi huu. Hata hivyo, kulingana na Neethan, kuwafurusha wakimbizi kwa nguvu ni kinyume na makubaliano ya Kenya na sheria za kimataifa na ya kuwa serikali itakiuka matkwa yake.

UNHCR inampa kila mkimbizi anayejitolea kurudi Somalia shilingi elfu kumi, huku kila familia wanaorudi kwa hiari ikipata shilingi elfu sitini. Zaidi ya hiyo, wakimbizi wanaorudi kwao wanapata vyakula kwa mda wa miezi tatu pamoja na mahitaji mengine kwa mda huo.