Idara ya huduma za misitu nchini ikishirikiana na mashirika mbali mbali waliendeleza shughuli ya kupanda miti siku ya Jumatano katika shule ya mafunzo ya makurutu katika Kaunti ya Uasin Gishu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Shughuli hiyo iliyoongozwa na naibu wa Gavana wa Kaunti ya Uasin Gishu Daniel Chemno,ilifaulu baada ya wafadhili kutoka mashirika mbali mbali kushirikiana na  kupanda miti elfu kumi na moja.

Akizungumza kwenye hafla hiyo,Kamanda wa shule hiyo ya mafunzo Juma Mwinyika aliwahimiza wananchi kupanda miti kwani mtu unaweza kuuza miti na kupata pesa na pia inavutia mvua.

Kamanda huyo aliwaambia wananchi kuwa,ukulima wa misitu itasaidia pakubwa kwa kuvutia wanyama ambapo watalii wataweza kutembea na hiyo itapandisha uchumi wa Kaunti ya Uasin Gishu.

Vile vile, Mwinyika alisema kuwa,shule hiyo ilianaza mpango wa askari wa mazingira mwaka wa 2006 na wamefaulu kupanda miti 358,721 hadi sasa.

Ana matarajio ya kupanda miti 40,000 mwaka huu katika shule hiyo.

Aidha, Paul Karanja ambaye ni afisa wa kutunza mazingira katika kaunti ya Uasin Gishu, alibainisha kuwa miti iliyokufa iliadhiriwa na ukame wala sio ugonjwa kama inavyosemwa na watu wengine.

Amewasihi wananchi kupanda miti itakayostahimili ukame kwa muda mrefu.

Karanja pia aliongeza kuwa badala ya wananchi kupanda miti kando kando ya shamba zao ili iwe kama uzio kwani pia miti hiyo itasaidia kukinga upepo mkali zaidi ya kuvutia mvua.