Wakaazi Mombasa wameulaumu upinzani kwa kukosa mwelekeo kwa sababu ya kupinga hata kisichostahili kupingwa.
Wakiongozwa na Khamisi Juma mmoja wa wakaazi hao, wamechoshwa na siasa za kila wakati na kuwaomba viongozi hao waambie wabunge wao wapeleke miswaada bungeni ambayo itafanya mwananchi wa kawaida kupata afueni kimaisha kama vile kushukishwa bei bidhaa muhimu nchini.
Vinara wa muungano wa upinzani Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula wamepuuzilia mbali hotuba ya rais Uhuru Kenyatta kwa taifa majuma mawili yaliyopita, wakiitaja kama iliyojaa ahadi zisizo na msingi.
Watatu hao wamesema kwamba Jubilee imeshindwa kuangazia matatizo yanayokumba wananchi wa kawaida, na badala yake wamekuwa wakiwahadaa wananchi kwa kipindi cha miaka mitatu tangu walipoingia uongozini.
Kauli hii ya upinzani imewadia wakati serikali ya Jubilee inaadhimisha miaka mitatu ya uongozi.