Wakaazi wa Solai wanalaani hali ya hewa na kuongezeka kwa joto huku usambazaji wa maji mijini ukidorora.
Mabishano pia yamezidi kuwa makali baina ya wakulima na wafugaji kuhusu matumizi ya vijito katika maeneo yao.
Taarifa nyingi za kitaalam siku za nyuma zilionya kuhusu uongezekaji wa mahitaji ya maji na viwango vya maji yanayopatikana lakini tahadhari hizo ama zilipuuzwa au hazikutiliwa maanani ipasavyo.
Mara nyingi wanasiasa walibeza tahadhari hizo bila kufikiri pale walipowapotosha wananchi wao kuvamia mazingira yaliyohifadhiwa ili wakate miti, kuanzisha makazi au kulima mashamba karibu na vyanzo vya mito.
Miji ambayo imepanuka kwa haraka katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa na vijito vingi, kama vile Kamukunji na Marram , sasa inapata adhari nyingi kuanzia mazingira machafu mpaka uhaba wa shughuli za kiuchumi kutokana na ukosefu wa maji. Wanalaani hali ya hewa na kuongezeka kwa joto wakati usambazaji wa maji mijini ukidorora na huku mabishano yakizidi kuwa makali baina ya wakulima na wafugaji kuhusu matumizi ya vijito katika maeneo yao.
“Uhai wetu, ustawi wetu, afya zetu na maendeleo yetu vyote hutegemea upatikanaji maji safi na salama pale tunapoishi. Wakati umefika tuone kila anayeharibu chanzo cha maji ni adui,” amesema Chifu wa Kata ndogo ya Marigu Simon Murage.
Hivi karibuni athari za kukauka kwa mito zimewasibu wananchi katika sehemu mbalimbali za Nakuru. Hata hivyo hakuna juhudi thabiti zinazofanywa na jamii au asasi za serikali kukabili athari zaidi za kimazingira, kijamii, kiuchumi na hata za kisiasa ambazo huenda zikasa ambazo huenda zikasababishwa na hali hii.
Watu wengi huharakisha kulaumu mabadiliko ya tabia nchi kwa kila mkasa hata kama wamekosa kuwa waangalifu wenyewe katika mwenendo wao wa maisha katika mazingiza yao.