Kamishina wa Kaunti ya Mombasa Maalim Mohammed amewahakikishia wafanyibiashara wanaoingiza na kutoa bidhaa zao humu nchini kupitia Bandari ya Mombasa usalama wa kutosha.
Akizungumza siku ya Alhamisi wakati wa kongamano kuu la baraza la maonyesho ya wauzaji wa bidhaa nje ya nchi, Maalim alisema kuwa hatua hiyo itasadia kuboresha sekta ya biashara na kukuza uchumi wa nchi.
Aidha, alisema kuwa pia wanatarajia kufanikisha uwekezaji hata katika matifa ya Afrika Mashariki.
“Ningependa kuwahimiza wafanyibiashara kushirikiana na maafisa wa polisi katika ukaguzi wa mizigo barabarani ili kuimarisha usalama wao na kuzuia kushuhudiwa kwa visa vya uhalifu,” alisema Maalim.
Kongamano hilo lilihudhuriwa na wadau katika sekta ya biashara kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni.