Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshirikishi wa eneo la bonde la ufa Wanyama Musiambo amewahikikishia wakaazi wa kaunti ya Nakuru usalama wao sawa na wageni wataohudhuria maombi ya shukrani hapo kesho Jumamosi katika uwanja wa wazi wa Afraha hapa mjni Nakuru.

Akiwa na wakuu wengine wa usalama kutoka vitengo mbalimbali vya idara za polisi , Musiambo ameeleza kuwa hali ya usalama Imeimarishwa katika mji wa nakuru na vitongoji vyake.

"Tumeweka miakakati yote na tunavyozungumza, kila jambo kuhusu usalama liko tayari. Usalama umeimarishwa kote mjini Nakuru," alisema Musiambo.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake mjini Nakuru Ijumaa, Musiambo aidha aalisema kuwa ifikapo saa nne usiku wa leo Ijumaa , maafisaa wa usalama watachukua uongozi wa mji wa Nakuru kikamilifu.

Aliongeza kuwa magari ya usafiri wa umma, magari ya kibinafsi, pikipiki hayataruhusiwa katikati mwa mji wa nakuru hapo kesho Jumamosi .

Badala yake, ametaja kuwa maeneo ya show ground mjini Nakuru, section 58 sawa na shule ya upili ya Menengai ndipo magari hayo ya usafiri wa umma yatakuwa yakiegeshwa huku wananchi wakilazimika kutembea kwa miguu kuingia hapa mjini Nakuru .

Magari ya masafa marefu pekee ndiyo yatakayoruhusiwa tu kupita katika barabara kuu za eneo hili wala si kuingia hapa mjini Nakuru.

Magari ya watu mashuhuri ndiyo pekee yataruhusiwa katikati mwa mji na yatakuwa na vibandikizo au stickers maalum kulingana na Musiambo.

"Magari yote hayataruhusiwa katikati mwa mji wa Nakuru. Hatutaruhusu pia baiskeli au pikipiki katikati mwa mji wa Nakuru. Tunawaambiwa wahudumu wa uchukuzi wa uma kuwa kuanzia leo jioni yale magari ambayo huwa katikati mwa mji wa Nakuru tnaomba yaondolewe," aliongeza Musiambo.

Kadhalika, ametoa onyo kwa wale ambao watakuja katika maombi hayo wakiwa wamevalia nguo zenye maandishi ya kisiasa, vyama au mabango ya kupigia upatu baadhi ya wanasiasa na wale wanaonuia kusimama katika uchaguzi mkuu ujao kuwa watachulukuliwa hatua kali.

Hata hivyo, Musiambo amewahakikishia wakaazi na wafanya biashara ya kuwa hakuna kukatizwa kwa shuguli zao siku hiyo ya kesho.