Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi ya wafanyibiashara katika mtaa wa Kibera wameshikilia kwamba wataendelea kuuza bidhaa muhimu kwa bei ya kawaida hadi pale akiba ya bidhaa waliyonayo kwa sasa itakamilika.

Wauzaji hao walisema haya siku moja baada ya serikali kuu kutoa mwongozo jumanne unaoonyesha kwamba bei za bidhaa kama vile sharubati, maji yanayopakiwa kwenye chupa na sigara miongoni mwa bidhaa nyingine.

"Tumepokea ripoti hiyo kwamba bei za sharubati, maji yanayoyouzwa kwenye chupa, na sigara zitapandishwa ushuru na hivyo kuongeza bei zao. Mimi nitaendelea kuza bidhaa hizo kwa bei ya kawaida hadi nitakapomaliza akiba niliyokuwa tayari nimeagiza," alisema Julliet Ochieng, mmiliki wa duka eneo la Olympic.

Eric Nyongesa anayeendeleza biashara ndogo ya kuuza sigara alisema kwamba kupandishwa kwa bei ya bidhaa hiyo ni njia mojawapo ya kuwanyanyasa wananchi wenye mapato ya chini, hasua wanaoishi katika mitaa ya mabanda.

"Kuna wale ambao wamezoea sigara kwa kiasi kwamba wataendelea kununua hata ikipindishwa bei. Hii inamaanisha kwamba watumiaji wa bidhaa hiyo watalazimika kutumia pesa zaidi na hivyo kuwatatiza kiuchumi," alisema Nyongesa.

"Kwa sasa nitaendelea kuuza sigara yangu kwa bei ya awali hadi nitakapoagiza nyingine," aliongeza.