Imebainika kuwa kaunti ya Mombasa iko na makundi takriban 30 ya kihalifu yanayowasumbua wakazi.
Haya ni kulingana na ripoti ya shirika la kijamii la KECOSCE lililopo mjini Mombasa.
Siku ya Jumatano, mkurugenzi wa shirika hilo Phyllis Muema alisema makundi hayo yanasumbua idara ya usalama katika kaunti ya Mombasa.
Aliongeza kuwa endapo idara ya usalama pamoja na jamii hawatashirikiana katika kuhamasisha vijana hao, basi huenda wakajiunga na makundi sugu ya kigaidi na kuanza kutumia bunduki.
Makundi hayo yanayopata msukumo kutoka kwa wanasiasa yapo zaidi katika maeneo ya Kisauni, Mvita na Likoni.