Mbunge wa Bomachoge Borabu Joel Onyancha ameutaka utawala wa kaunti kuweka wazi miradi ya maendeleo wanayoishughulikia ili kuepusha mirundiko ya marudio ya uwekezaji wa miradi sawia kutoka kwa hazina ya maendeleo ya maeneo bunge na malengo ya serikali kuu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kiongozi huyo alikuwa akiyasema haya wakati wa kufanya kiakao na mwakilishi wa wadi ya Ibencho George Bibao katika eneo la kenyenya siku ya Jumamosi, ambapo kulikuwa kumezuka lawama kuhusu miradi ya maendeleo inayotamaniwa na wenyeji wa eneo bunge la Bomachoge Borabu.

“Hatuwezi kukimya na tushinde tukifanya marudio ya miradi ya maendeleo kutoka kwa sekta husika ilhali mwananchi yuahitaji mengi kutoka kwa viongozi waliochaguliwa,” alisema Onyancha.

Miradi ya miundomsingi hasa barabara imekuwa ikiwakanganya wengi kuhusiana na ni nani alaumiwe kwa kutoundwa kwa barabara hizo, hasa ikizingatiwa kuwa kila kiongozi aliyekuwa akitafuta kura alikuwa na ahadi sawia za kuimarisha hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida.

Kulingana na Onyancha, kila kitengo na kiwajibikie utendakazi wake ili umakinifu uwe, kando na kuepusha siasa za mvuto kufanya maendeleo kwa ubaguzi.

“Sioni haja ya serikali ya kaunti kushinda ikipanua barabara ndogondogo ilhali umuhimu wake haupo kabisa na kuacha barabara zinazofaa kukarabatiwa kurahisisha usafiri,’ aliongezea Onyancha.

Alihoji kuwa huenda kukazuka na sakata kubwa na mbaya zaidi ikiwa ugatuzi hautaeleweka vyema, na wanaofaa kuhakikisha umeafikiwa kwani upeanaji wa kandarasi hasa za barabara za wadi umekumbwa na kizungumkuti kila kuchao, huku wananchi wakidai kuwa baadhi ya wawakilishi wa wadi hupewa hela za kufanya miradi ambayo haipo ili kuweka mfukoni hela za kaunti na hongo kutulia wasimpige vita gavana.

Diwani mteule katika kaunti ya Kisii ambaye pia alihudhuria mkutano huo Esther Nyamwamu alidai kuwa wenzake ambao wamepigiwa kura huwa wanapokea kushughulikiwa kwa mapema kwa kila kitu dhidi yao,

“Tuko hapo tu, wenzetu waliochaguliwa huwa wanapewa hela nyingi kila mara wanamtishia gavana kuwa watamuondoa mamlakani kwa njia ya kupewa hela kufanya miradi ghushi,” alisema kiongozi huyo.