Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga akiwahutubia wakaazi katika hafla ya awali. Picha/ the-star.co.ke
Ukosefu wa ushirikiano miongoni mwa viongozi wa ukanda wa Pwani umechangia eneo hilo kudharauliwa na hata kukosa maendeleo.
Haya ni kwa mujibu wa Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga.Mbunge huyo alisema kuwa hali ya viongozi kutofautiana kwa misingi ya kisiasa imechangia kudidimia kwa maendeleo katika ukanda huo.Akizungumza na wanahabari mjini Mombasa, mbunge huyo alisema kwamba endapo viongozi wa Pwani watashirikiana vyema na kuwaelekeza wakaazi katika misingi bora bila kuwagawanya katika misingi ya kisiasa, basi eneo la Pwani litapiga hatua za kimaendeleo.Mwinga alisema kuwa kuna haja ya viongozi wa Pwani kujitenga na kasumba ya vyama, kwani hali hiyo imechangia kushuhudiwa kwa utengano baina yao na hata kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wakaazi.Wakati huo huo, amewataka wakaazi wa Pwani kuwachagua viongozi bila kuegemea chama chochote, na kusema kuwa hiyo ndiyo njia ya pekee ya kuleta maendeleo na uchumi katika ukanda huo.