Mbunge wa Kisauni amezindua mradi wa ujenzi wa kiwanja kipya cha kisasa katika eneo la Baptist Mlaleo.
Akizungumza alipozuru uwanja huo siku ya Jumamosi, Rashid Bedzimba alisema kuwa kiwanja hicho ambacho kinanuiwa kujengwa kwa mbinu za kisasa, kitawawezesha vijana kukuza vipaji na talanta zao.
"Nataka kuwasihi vijana kuchukua fursa hii ili kukitumikia vilivyo uwanja huu utakapomalizika,” alisema Bedzimba.
Mbunge huyo alikuwa ameandamana na mwakilishi wa Joho al maarufu kama Alfa 00A na mwanasiasa anayewania kiti cha uwakilishi wadi ya Magongoni Omar Bedzimba.