[Mwanamuziki wa Bongo, Vanessa Mdee. Picha/Tanzania Now] 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwezi jana, mwanamuziki mashuhuri Afrika Mashariki, wa Tanzania (Tzee) Vanessa Mdee, alijikuta kati ya wenzake, waliyoshukiwa kuwa walanguzi wa dawa za kulevya. 

Hii ni baada ya serikali ya Rais John Pombe Magufuli kutoa onyo kali kuhusu ulanguzi na walanguzi wa dawa hizo, kwa kutoa orodha ('listi') ya watu waliyokisiwa kujihusisha na biashara hiyo haramu. 

Mpenzi wa zamani wa Diamond Platinumz, Wema Sepetu, Diamond mwenyewe, Babu wa Kitaa, na TID ni baadhi tu, ya wanamuziki wa Bongo, waliyokuwa kwenye listi moja na Mdee. 

Hata hivyo, ripoti zasema kuwa Mdee alikuwa safarini kulekea Afrika Kusini, ku'pafomu', listi hiyo ilipotoka. 

Ilimbidi apinduke na kuripoti kwenye afisi husika kwenye serikali, baada ya kuitwa mara moja! 

Baadaye, alitiwa mbaroni na kutiwa korokoroni, Dare es Salaam, aliko'spendi' usiku mmoja. 

Kulingana na Mkuu wa eneo, Tzee, Paul Makonda, jina la Mdee halikupatikana kimakosa kwenye listi hiyo, maana kulikuwa na ushahidi tosha, uliyomhusisha na ulanguzi na utumiaji dawa za kusisimua misuli. 

Baada ya kuripoti kwenye afisi za polisi, muimbaji huyo wa 'Niroge' alipelekwa kwenye afisi za Mkuu wa Dawa kwa uchunguzi zaidi. 

Polisi walikuwa tayari wamekagua nyumba yake, kutafuta ushahidi zaidi. 

Ripoti zaidi kutoka Tzee zilisema uchunguzi bado waendelea kuhusu kisa hicho. 

Hata hivyo, Diamond alikanusha madai kuwa yeye ni mmoja wa walanguzi wa dawa za kulevya. 

Alizungumza kwenye 'show' ya Mambo Mseto, Kenya.