Afisa wa usalama katika kaunti ya Kisii Patrick Lumumba, amewashauri vijana katika kaunti hiyo kufanya kilimo.
Lumumba amesema kuwa hatua hii itasaidia kupunguza ukosefu wa chakula katika eneo hilo.
Akizungumza na wanahabari hiyo jana katika mji wa Kisii Lumumba, alisema vijana wengi wamezembea kazi ya ukulima.
“Vijana wengi wamezoea kukaa bure huku wakisema hakuna kazi ilhali wanaweza fanya kazi ya ukulima,” asema Lumumba.
Aidha, afisa huyo aliwashauri vijana kuwekeza katika kilimo cha mboga.
“Hatuna mboga za kutosha katika kaunti yetu. Mara mingi huwa tunapokea mboga kutoka kaunti njirani. Vijana wanapaswa kuingilia kilimo na watapata pesa,” akasema Lumumba.
Lumumba aliwaomba vijana kujihusisha na kilimo cha kahawa, mboga na nyanya ili kujiendeleza kimaendeleo na kuimarisha maisha yao.
“Viwanda vya kahawa katika eneo la Kirinyaga hupokea kahawa nyingi na kutengeneza majani chai, mbona eneo letu la Kisii ambalo hupokea mvua nyingi kwa mwaka tusiwe na kahawa ya kutosha,” auliza Lumumba.
Afisaa huyo alisema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuona kuwa vijana wengi katika kaunti hiyo hushida wakizurura ilhali wanaweza fanya kilimo.