Vijana katika kaunti ndogo ya Molo watanufaika na maduka kutoka kwa serikali ya kaunti katika mradi wa kuwainua vijana.

Share news tips with us here at Hivisasa

Maduka hayo yalizinduliwa hii leo na gavana wa kaunti hiyo Kinuthia Mbugua.

“Tumezindua maduka haya kuwasaidia vijana walio kwenye makundi,” Kinuthia alisema.

Kinuthia alitoa maduka hayo Ijumaa alipokuwa akiwaahudumia wakaazi wa kaunti ndogo ya Molo kupitia huduma ya ‘Gavana mtaani.’ “Tutahakikisha kuwa maduka hayo ishirini yametolewa pasi mapendeleo yoyote ili kufaidi vikundi vyote,” aliongeza Kinuthia.