Wito huo ulitolewa siku ya Jumatano na kiongozi wa vijana kwenye Wadi hiyo, Hillary Juma ambaye alikua ametembelea makundi ya vijana walio na miradi mbali mbali katika eneo hilo.
“Jamani vitambulisho viko na yeyote asije akaachwa nyuma kwa sababu zozote zile. Serikali imejitolea kuwapa vijana vitambulisho, na hivo basi tusikose kushiriki zoezi hili ambalo linaendela kwa sasa katika Kaunti yetu,” alisema Juma.
Kiongozi huyo wa vijana alihoji kwamba vijana wengi huachwa nje wakati wa kupiga kura kwa sababu hawana vitambulisho. Alisema kuwa kukosa kushiriki kwenye uchaguzi wa viongozi nchini ni kukosa haki ya kitaifa kikatiba.
“Uchaguzi unapofika ni sheria ya kikatiba kwa kila mwananchi ambaye amehitimu umri wa miaka 18 na zaidi kushiriki zoezi la uchaguzi wa viongozi wa nchi yake,” alisema Juma.
Aidha Juma liwataka viongozi wa utawala wakiwemo Chifu na Naibu wao kurahisisha zoezi hilo kwa kuwatangazia wananchi katika maeneo yao kupitia hata kwenye baraza zao, akisema kuwa wengi huachwa nje wakati kama huu kwa sababu wanakosa kufahamishwa na kuhamazishwa.
“Nawasihi viongozi wote wa utawala wakiwemo Machifu na manaibu wao kuwatangazia wananchi popote kwenye baraza zao kujitokeza kushika vitambulisho, kwa kuwa wengi huachwa nje wakati kama huu kwa sababu za kutokufahamishwa yanayojiri,” alisema Juma.