Vijana katika kaunti ya Mombasa wamehimizwa kuwaacha kutegemea kazi za kuajiriwa na badala yake kuwa wabuni wa ajira binafsi ili waweze kujiendeleza maishani.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akitoa mwito huo, Afisa wa Haki na Sheria katika Shirika la Utetezi wa haki za kibinadamu nchini la Haki Afrika Francis Auma Gamba alisema kuwa vijana wengi hutarajia kazi za kuajiriwa ilhali hawana viwango vinavyohitajika vya masomo.

Akizungumza katika kongamano la vijana katika hoteli moja mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Auma alisema kuwa hali hiyo iliwaacha vijana wengi bila ya ajira, ambapo wengine wao hujiingiza kwenye makundi yenye itikadi kali.

Auma aliwahimiza vijana watafute ushauri kutoka kwa viongozi kuhusu kujiendeleza katika masuala ya biashara ili kuwawezesha kubuni ajira na kujikimu kimaisha.

“Tunawaomba vijana tafadhili kuweni wabunifu wa ajira badala ya kusalia kusubiri kuajiriwa mara nyingi ajira hizo zikitangazwa huwa zinahitaji viwango vya juu vya masomo na wengi wenu huwa hamna lakini mkichukua wazo hili basi mtajitenga na maovu mengi na kujiendeleza maishani,” alieleza Auma.