Vijana katika Kaunti ya Mombasa wameonywa dhidi ya kutumiwa na wanasiasa wakati huu ambapo msimu wa kampeni unawadia.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Jumatano, Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki, aliwahimiza vijana kujihusisha na mawsala ya maendeleo yatakayo wasaidia kujiimarisha kimaisha kama vile biashara.

Aidha, aliwaonya vijana dhidi ya kujihusisha na utumizi wa dawa za kulevya na makundi ya kigaidi, kwa kusisitiza kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria.

Vile vile, amewataka vijana kujihusisha na maswala ya usalama na kutoa ripoti kwa ofisi za usalama wakati kuna tatizo mahali.