Mwakilishi mteule wa wadi katika bunge la kaunti ya Nakuru Rosemary Wanjiru Okemwa ametoa wito kwa vijana wa kaunti kujitokeza na kupata taarifa muhimu kuhusu maswala ya vijana katika kaunti ya Nakuru.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katika kikao na wanahabari mjini Nakuru, MCA Okemwa anasema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba vijana wa Nakuru wanakosa kujihusisha katika uongozi.

"Vijana ni lazima wajitokeze na kujihusisha na uongozi wa kaunti hii. Matatizo ya vijana yatapata suluhu iwapo watajihusisha na maswala kwenye kaunti hii," Wanjiru alisema.

Mwakilishi huyo mteule kutoka wadi ya Biashara ametoa wito kwa wazazi kuwa kielelezo kwa watoto wao. 

Ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kwa watoto kukosa mwelekeo ilhali wapo wazazi wa kuwapa mwelekeo.

"Wazazi pia nawatolea changamoto kuwa kielelezo muhimu kwa watoto wetu. Tukifanya hivyo, tutakuza kizazi cha vijana walio na msingi," aliongeza.

Vijana mjini Nakuru wamekuwa wakiteta kutengwa na serikali ya kaunti hiyo katika utoaji wa nafasi za kazi.