Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kikundi cha vijana kwa jina North Mugirango Scholars Association kutoka eneo bunge la Mugirango Kaskazini kaunti ya Nyamira, kimeanzisha kampeini ya kuwashawishi vijana kujiandikisha kwa wingi kupata kadi za kupiga kura ili kujitayarisha kuwachagua viongozi ambao watawafanyia maendeleo katika uchaguzi ujao.

Wakizungumza na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumapili katika eneo la Manga, mwenyekiti wa kikundi hicho Erick Mwereza na katibu wa kikundi hicho Abel Ongeri walisema waliamua kuanzisha kampeini hiyo ili vijana waweze kujiandikisha ili kupata kadi za kupiga kura na kuwachagua viongonzi ambao watawasaidia vijana haswa kimaendeleo.

“Viongonzi walio katika mamlaka sasa hivi hawajali wala hawakumbuki vijana. Ndio maana tukaamua tuanzishe kampeini hii ili vijana wajiandikishe tuchague viongozi watakaojali maslahi yetu kwanzia hapa kwa eneo bunge mpaka kwa serikali kuu,” alisema Erick Mwereza.

“Naomba vijana tuungane pamoja ili tubadilishe uongozi wa eneo bunge hili la Mugirango Kaskazini ili uongozzi huo uwe wa kisasa,” aliongeza Mwereza.

Wakati huo huo katibu wa kikundi hicho Abel Ongeri alisema vijana watachangia pakubwa kimaendeleo ikiwa watashikana pamoja katika eneo bunge hilo.

“Naomba wajiandikishe kupata kadi za kura katika eneo bunge letu na wasidanganywe kujiandikisha kwa maeneo bunge mengine. Wajiandikishe hapa nyumbani ili tubadilishe uongozi,” alisema Ongeri.

Tumejitayarisha vilivyo ili tufanye biashara na miradi mingine tutakapopewa pesa za vijana ili eneo letu liinuke kimaendeleo,” aliongeza Ongeri.