Vijana katika eneo la Pwani wameshauriwa kujiepusha na siasa za chuki, ukabila na kidini na badala yake kujitenga na viongozi waliyo na azma kama hiyo ili kuhakikisha taifa hili liko salama.

Share news tips with us here at Hivisasa

Afisa mratibu wa mipango katika Shirika la kijamii ‘Kenya Community Support Centre’, Hassan Kibwana mara nyingi vijana hutumiwa vibaya na viongozi wa kisiasa na kuanza kutofautiana.

Akizungumza katika mkutano wa vijana mjini Mombasa siku ya Jumanne Kibwana amewataka kuwa na uiano na utangamano na kufanya siasa kwa njia ya amani hasa Wakenya wanapokaribia katika mchakato wa kisiasa na kampeni za kisiasa huku akisema kuwa iwapo vija watapata wawakilishi katika bunge la kitaifa basi maswala ya kiamendeleo yatatekelezwa vyema.

Wakati uo huo Kibwana amewarai vijana wanalenga kujitosa katika ulingo wa kisiasa ili kuchaguliwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao kushikana mkono na vijana wenzao ili kubadilisha uongozi wa taifa hili.

"Ninawaomba vijana wanalenga kujitosa katika ulingo wa kisiasa kuwa makini na kujiepusha na siasa za chuki ili kuwawezesha vijana wengine kudumisha amani na utangamano," alisema Kibwana.

Mwanaharakati huyo wamewahimiza vijana kuhakikisha kuwa wanadumisha amani ili taifa hili kuwa na usalama wakutosha.