Serikali Kuu imeanzisha mradi mpya wa Jua Kali mjini Kisii ambao umekuwa ukididimia kwa muda mrefu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mji wa Kisii, msimamizi wa shirika la Micro and Small Enterprise Authority Patric Mwangi alisema kuwa Sekta ya Jua Kali imekuwa ikisahaulika kwa muda mrefu na kusababishiwa kudidimia.

Msimamizi huyo alisema kuwa uongonzi wa shirika la Jua Kali umekuwa mbaya zaidi na kuomba vijana wa umri mdogo kujiunga na sekta hiyo ili uchaguzi ukifanywa kwenye sekta hiyo wachaguliwe kuwa viongonzi kama njia mojawapo ya kuinua sekta hiyo juu.

“Kuna wazee ambao wamekwamilia katika uongonzi wa Sekta ya Jua Kali na nahimiza vijana wajiunge na Sekta ya Jua Kali,” alihoji Mwangi.

Wakati uo huo msimamizi huyo alieleza kuwa sekta hiyo ilianguka kwa sababu ya ukosefu wa sheria inayoisimamia sekta hiyo ambayo amesema kuwa intengenezwa.

“Sekta ya kiufundi humu nchini iko juu zaidi na Serikali tayari imeweka mikakati kabambe ya kuinua ufundi zaidi ili vijana waweze kujiimarisha na kujiendeleza kimaisha,” aliongezea Mwangi.

Vijana wote sasa wameombwa kutengeneza vikundi vyao na kujiingiza katika sekta hiyo ili waje wakanufaike zaidi katika siku sijazo.