Maandamano yalishuhudiwa mjini Kisii siku ya Jumatano kulalamikia kuzuiliwa kwa mwanasiasa Don Bosco Gichana nchini Tanzania.
Waandamanaji hao waliomba serikali ya kaunti ya Kisii ikiongozwa na gavana James Ongwae pamoja na serikali kuu kushirikiana na kuelekea nchini Tanzania ili mwanasiasa huyu aachiliwe huru na kurudi nyumbani Kenya.
Mwanasiasa huyu alitiwa mbaroni kwa madai ya ulaghai, jambo ambalo liliweza kumfanya kuzuiliwa nchini humo.
Waandamanaji hao wakiongozwa na Hezekia Mobisa ambaye alizungumza na waandishi wa habari siku ya juamatano mjini Kisii alisema kuna watoto wengi ambao walikuwa wanasomeshwa na mwanasiasa huyo nchini ya muungano wake kwa jina Don Bosco Foundation na hawajawai enda shule tangu azuiliwe nchini Tanzania kwa ukosefu wa karo.
“Tunahitaji Bosco arudi Kenya ili watoto wale alikuwa anawasomesha waendelee na shule mbona Bosco anazuiliwa bila haki? aliuliza Hezekiah mobiza kiongozi wa waandamaji.
Waandamanaji hao walitishia kuelekle nchini Tanzania ikiwa Rais Jakaya Kikwete hatamwachilia huru huku wakiomba serikali ya kaunti ya Kisii na ya kitaifa kuungana pamoja kuhakikisha mwanasiasa Gichana ameachiliwa kabla ya Rais tofauti kuchukua mamlaka nchini tanzania.
Miongoni mwa wanafunzi ambao walisema kuwa tangu mwanasiasa huyo afungwe hawachawai enda shule ni Richard Moseti, Shem Ombae, Sara Ontiri miongoni mwa wengine.
Wanafuzi hao walidai kuwa mwanasiasa huyo amezuiliwa bila haki kutendeka dhidi yake
Mwanasiasa huyo aliwania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Kitutu Chache Kusini kupitia chama cha People’s Democratic Party (PDP) na akapoteza kura kwa mbunge Richard Momoima Onyonka na akachukuwa nambari ya pili.