Vijana kutoka eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini kaunti ya Kisii, wameanzisha chama chao kwa jina Kitutu Chache Noth association ambacho kitawaleta vijana waeneo hilo pamoja.
Chama hicho kilizinduliwa jana katika shule ya wasichana ya Marani iliyoko wadi ya Marani eneo bunge la kitutu chache kaskazini huku Boas Makori akichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
“Sisi chama chetu hakijihusishi na siasa lakini tunataka kufadliwa na wanasiasa ili tuweze kujiimarisha kimaendeleo,” alisema Makori.
Viongozi mbalimbali wakisiasa walihudhria hafla hiyo iliyoandaliwa ijumaa.
“Hii ni njia mojawapo ya kuwaleta vijana wa eneo bunge hili pamoja ili tupokezane mafunzo ya jinsi ya kuishi kama vijana na kujiimarisha kimaisha,” alihoji Makori.
Chama hicho sasa kimewaarika vijana wa eneo hilo kujiandikisha ili kujiendeleza kimaendeleo na kujua mambo wanapaswa kuwa wanafanya.
“Mimi mwenyewe nafurahia kwa sababu ya chama hiki. Ingawa hatutajihusisha na maswala ya siasa tutaweza kuendeleza maisha yetu kwa pamoja,”akasema Antony Masaka mwana chama.
Pamoja na wale walihudhuria ni mwakilishi wa vijana katika bunge la Kisii Omengo Ochieng pamoja na mwakilishi wa wadi hiyo Evans Makori.
Mwakilishi wa wadi ya Sensi Ochon’a Nyagaka,mwakilishi wa wadi ya marani Denis Ombachi pamoja na mwakilishi wa kaunti ya Kisii Mary Otara hakwauweza kuhudhuria ingawaje walikuwa wamealikwa