Vijana ambao hawajafanikiwa kujiunga na chuo kikuu, na wale waliositisha masomo yao wametakiwa kujiunga na vyuo vya Anuai kama njia moja ya kujiendeleza kimaisha, sawia na kutakiwa kuomba kandarasi katika serikali za jimbo ili kujiimarisha kiuchumi.
Haya ni kwa mjibu wa katibu katika wizara ya elimu, vijana na utamaduni katika jimbo la Nakuru Joseph Tonui.
Asilimia thelathini iliyotengewa kina mama, vijana na hata walemavu ni ya kuwasaidia kujiinua na kujiendeleza kimaisha, hii ndio sababu kuu ambayo nasisitiza haya, kuwa vijana wajisajili katika vikundi kama njia moja ya kuwawezesha kunufaika kwa kupata kandarasi hizo,” alisema Tonui akiwa ofisini mwake.
Aidha, Tonui amewataka vijana walio na talanta mbalimbali kama kuimba, kuigiza sawia na riadha kujitokeza ili waweze kupata msaada wa kuinua vipaji zao.
Vijana wengi wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa ajira, huku wengine wakiamua kuingilia madawa za kulevya na uhalifu ili kujikimu kimaiasha.