Vijana katika kaunti ya Mombasa wamehimizwa kuwa wabunifu wa ajira ili kufaidika na miradi mbalimbali ambayo serikali kuu na ile ya kaunti inalenga kuanzisha.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mwenyekiti wa kamati ya bunge la kaunti ya Mombasa kuhusu vijana, michezo na jinsia Serah Nyamvullah alisema kuwa iwapo vijana hao watatekeleza fikra hizo basi watanufaika zaidi na kuwawezesha kujikimu kimaisha.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Alhamisi kwenye mkutano wa vijana, Nyamvullah alisema kuwa tayari serikali ya kaunti hiyo kwa ushirikiano na serikali kuu imeanzisha mpango huo wa kuwakimu vijana kimaisha huku akiwahimiza vijana hao kuungana katika makundi.

Alisema kuwa vijana wengi hupuuza mipango hiyo na kujihusisha na maswala ya utumizi wa mhadarati na uhalifu kutokana na kuwa wengi wao hawajapata hamasa kuhusu mapango wa kujiajiri wenyewe.

“Tunawahimiza vijana wengi kutosalia katika maskani na kujihusisha na mambo yasiofaa la msingi ni kujiunga katika makundi na kuwa wabunifu wa ajira na serikali yakaunti ya ile kuu itawasaidia kuwawezesha kutimiza malengo yao na kujikimu kimaisha,” alisema Nyamvullah.

Tayari baadhi ya vijana wameanza kujitokeza na kubuni makundi ya vijana ili kufaidika na mpango huo wa serikali ya kaunti na ile serikali kuu na kufanikisha ndoto zao.