Vijana na kina mama katika eneo bunge la Mvita wametakiwa wajiunge kwenye vikundi ili wafaidi na mikopo ya hazina ya Uwezo.
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesema kuwa yuko tayari kusaidia vikundi hivyo kuimarika zaidi katika miradi yao na biashara mbali mbali.
Aidha, alionyesha kusikitishwa kuona kuwa kumesalia shilingi milioni tano ambazo hazijachukuliwa katika jumla ya shilingi milioni 15 alizotengewa na serikali.
Aliyasema hayo siku ya Jumanne alipozuru vikundi kadhaa vya vijana na kina mama vilivyofaidi na mikopo hiyo inayotolewa bila riba ili kuona miradi waliyonzisha.
Zaidi ya makundi 100 ya vijana kutoka eneo bunge hilo yamefaidika na mikopo ya hazina ya uwezo katika jumla ya shilingi milioni 15 zilizotengewa eneo hilo na serikali ya kitaifa.
Picha: Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir. Amewarai vijana na wanawake kutoka eneo lake kuhakikisha wamejiunga kwa makundi ili kupokea ufadhili kutoka kwa serikali. Maktaba