Vijana wanne wamefikishwa kizimbani kwa kosa la kutekeleza wizi wa mabavu.
Mahakama ilielezwa siku ya Alhamisi kuwa Stephen Owiti Ngandi, Ali David Morage, Brian Nguro Kariuki na Mwalimu Suleiman Mwendo, wakiwa wamejihami kwa visu na mapanga eneo la Shelly Beach huko Likoni, wanadaiwa kumuibia Bidalla Peru Mwajaamanda, simu yenye thamani ya shilingi 15,000 na pesa taslim 2,590.
Aidha, wanadaiwa kutishia kumjeruhi mlalamishi wakati wakitekeleza kitendo hicho.
Wakati uo huo wanadaiwa kuiba simu ya thamani ya 8,000 na pesa taslim shilingi 6,600 mali ya Fatuma Salim, katika eneo la Shelly Beach huko Likoni.
Wote wamakanusha madai hayo mbele ya hakimu katika mahakama ya Mombasa, Diana Mochache.
Hakimu amewaonya washtakiwa kuwa iwapo watapatikana na hatia hukumu yao uwa ni kifo kwa mujibu wa katiba.
Mahakama imewaachilia kwa dhamana ya shilingi 500,000.
Kesi itasikilizwa Juni 16, 2016.