Share news tips with us here at Hivisasa

Balozi wa serikali ya Kenya Samson Ongeri amewaomba vijana kusaidia serikali kutekeleza miradi mbalimbali.

Akizungumza siku ya Ijumaa alipohudhuria mazishi katika eneo bunge la Nyaribari Masaba, Ongeri aliwaomba vijana kuisaidia serikali ya kaunti hiyo na ile kuu katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

"Nawaomba vijana mutumie njia zifaazo kutatua mizozo kati yenu na serikali na muwe katika mstari wa mbele katika kuendeleza miradi ya maendeleo ili kuimarisha maisha ya wakenya kwa jumla," alisema Ongeri.

Aidha, Ongeri aliwaonya vijana dhidi ya biashara ya kuuza pombe haramu nchini akisema pombe hiyo huleta uzembe na umaskini nchini na katika maeneo ambayo imekidhiri.

Ongeri pia aliwaomba machifu wote wa eneo la kisii kuwajibikia kazi yao na kuimarisha na kutekeleza amri ya Raisi Uhuru Kenyatta huku akisema kuwa amri hiyo inalenga kuwasaidia vijana na kuwaendeleza kimaisha.

Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa wadi ya Gesusu kaunti ya Kisii, Sammy Keronche pia aliwaataka wakazi wa eneo hilo kuunga mkono viongozi wote nchini ili kuleta uwiano na maendeleo katika eneo hilo.

"Tufanye kazi pamoja kama jamii ya mkenya ili amani idumu miongoni mwetu kwa kuwa sisi kama viongozi tunahitaji usaidizi wenyu ili tuweze kuendelea kama taifa letu tukufu la kenya," alisema Keronche.