Vijana kutoka Kaunti ya Nyamira waliofanya mtihani na kupokea matokeo yao hivi majuzi wameombwa kujiunga katika taasisi za ufundi ili kujiendeleza kimaisha.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea hii siku ya Jumanne alipozuru taasisi ya Enchoro, waziri wa elimu kaunti ya Nyamira Peter Omwaza alisema kuwa taasisis hiyo itageuzwa kuwa ya kisasa ili kushgllikia mahitaji ya wanafunzi.

Vilevile, serikali hiyo imeahidi kujenga mabweni katika taasisi hiyo, ili kuwarahisishia kazi wanaotaka  kujiunga.

Kulingana na mwenyekiti wa taasisi hiyo Peter Minyira, wana wanafunzi zaidi ya 150, na wnataraji kuongeza idadi hiyo.

“Taasisi hii ina vifaa vya kutosha na itasaidia pakubwa na kuinua viwango vya masomo katika eneo  hili,” alisema mwenyekiti.

Kulingana na wakaazi wa lokesheni ya Mochenwa, vijana wengi hupuuza masomo baada ya kufanya kidato cha nne na kupata matokeo duni, na kujihuzisha katika vileo na ndoa za mapema.

Aidha, wameowaomba vijana hao kuingia katika taasisi na  kupokea masomo ili kujinufaisha kimaisha.

”Vijana wengi hupuuza masomo zaidi kwa kutojali maisha yao ya kesho kutokana na wazazi wao kutowaelekeza  kwa njia bora,” alisema mzee mmoja wa kijiji.

Wanafunzi wengi wanaopata masomo katika taasisi ya ufundi wanatoka  maeneo  mengine, kitu kinachowatia moyo wakaazi hao kuwapa motisha wanao.

Kulingana na wasimamizi wa taasisi hiyo, kwa sasa kuna vifaa vya kutosha na waathiri wanao tajiriba ya juu.