Msanii wa ucheshi kutoka kaunti ya Nakuru Kelvin Omwami amewatahadharisha vijana katika kaunti ya Nakuru na taifa kwa jumla dhidi ya kukubali kutumiwa vibaya na wanasiasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Katika mahojiano, Omwami ambaye pia hushiriki kipindi cha 'Churchil show', amewataka vijana kutumia vyema talanta.

"Vijana wana talanta na wanafaa kuzitumia vyema badala ya kungoja kutumiwa vibaya na wanasiasa" Omwami alisema.

Wakati huo huo,Omwami alitoa wito kwa vijana kujisajili kwa wingi kama wapiga kura ili kushiriki uchaguzi mkuu ujao.

Kwa mujibu wake, vijana wanaweza leta mabadiliko iwapo watapiga kura bila kushrutishwa.