Share news tips with us here at Hivisasa

Vijana wa dhehebu la PCEA Dr.Arthur mjini Nakuru wametakiwa kuwa kielelezo katika maadili ya vijana humu nchini.

Wito huo ulitolewa na mchungaji Denis Kamau Kamande ambaye anasema kuwa vijana ni nguzo muhimu na watainua taifa hili iwapo watazingatia maadili ya mwenyezi Mungu.

"Taifa hili, asilimia kubwa ni vijana na wanafaa kuwajibika, kuishi kulingana na maadili ya mwenyezi Mungu na hata kubadili vijana wenzao ambao hawana mwelekeo" Kamande alisema.

Akizungumza katika ibada ya Jumapili katika kanisa la PCEA Dr Arthur, Kamande pia aliwataka wazazi wazidi kuwaombea watoto wao ili kuepuka changamoto.

Kwa mujibu wake,vijana wanapitia changamoto si haba lakini wanaweza kufaulu kupitia maombi.

Vijana wa PCEA Dr Arthur wakipigwa picha baada ya wao kuongoza ibada ya jumapili.Wamehimizwa kuwa kielelezo katika jamii.PRISTONE MAMBILI/Hivisasa.com