Jengo la mahakama ya Mombasa. [samawatilive.co.k]

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vijana wawili wamefikishwa katika mahakama kuu ya Mombasa kwa madai ya kumuuwa baba yao huko kaunti ya Kwale.

Katana Mwaringa Katana mwenye umri wa miaka 17 na Chirima Ndurya mwenye umri wa miaka 20 wanadaiwa kumuuwa Mwaringa Katana mnamo  Januari 16,2018 katika eneo la Vgurungani kaunti ya Kwale.

Washukiwa wanadaiwa kuchukuwa hatua hiyo baada ya baba yao kudida kuuza Ng’ombe za familia.

Washukiwa hao hawakusomewa mashtaka baada ya afisi ya mwendesha mashtaka kutaka wawili hao kupimwa akili katika hospitali ya Makadara.

Afisi ya mwendesha mashtaka tawi la Mombasa imemtaka jaji Dora Chepkwonyi kuagiza washukiwa kuzuiliwa katika gereza la Shimo La Tewa.

Jaji Dora ameagiza wawili hao watazuliwa katika gereza la Shimo La Tewa.

Kesi yao itatajwa Februari 14, 2018.