Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vijana katika zoezi la kuwasajili makurutu hapo awali. [Picha/ the-star.co.ke]

Idadi kubwa ya vijana wamekosa kufuzu kwenye zoezi la kusajili makurutu kutokana na vimo vyao vifupi.Kulingana na masharti ya Idara ya Polisi, sharti makurutu wawe na urefu wa zaidi ya futi 5.5.Wakizungumza siku ya Alhamisi katika uwanja wa maonyesho ya kilimo eneo bunge la Nyali, baadhi ya vijana wenye vimo vifupi walisema kuwa wamesikitishwa na hatua hiyo ya kufungiwa nje ya zoezi hilo kwa sababu ya maumbile yao.Hussein Athuman aliitaja hatua hiyo kama ya maonevu, na kusema kuwa maumbile hayapaswi kuwa kikwazo kwake kukosa kujiunga na idara hiyo ya polisi.Hussein amewataka wakuu wa polisi kupunguza viwango hivyo vya urefu na badala yake kuangalia uwezo wa mtu wa kuhudumu katika idara hiyo.“Kimo sicho ambacho kitashika bunduki ama kulinda usalama. Kimo ni maumbile ya Mungu na hatuwezi mlaumu kwa jinsi alivyotumba,” alisema Hussein.