Wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Nyamira hawajafurahishwa na shinikizo la muungano wa upinzani, Cord, ambao unasisitiza kuwa wakuu wa bodi ya uchaguzi na mipaka (IEBC) waondelewe afisini. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Haya yamejiri baada ya wawakilishi hao ambao wanawalaumu vinara wa Cord kuwa hawafuati sheria na kanuni za katiba hili waweze kuwaondoa afisini kisheria.

"Kuna sheria mwafaka ambazo zimeidhinishwa katika katiba ya Kenya na tumegundua kuwa muungano wa Cord haujafuata sheria," alisema mkazi mmoja.

"CORD wasipokuwa makini huenda wakajiharibia kura zao za mwaka ujao. Kwa hivyo tungependa kuwatahadharisha kuwa walichukulie jambo hili kuwa la dharura," waliongezea wakazi.