Share news tips with us here at Hivisasa

Viongonzi na wanasiasa wote katika kaunti ya  Kisii wameombwa kutowapa vijana pesa bali watumie pesa hizo kuanzisha academia ya michezo.

Vijana wakijiunga na academia hizo, watapata fursa ya kujua na kugundua talanta zao ambazo zitawasaidia katika siku za usoni. 

Akizungumza siku ya Jumapili katika mji wa Nyaturago ulioko eneo bunge la Nyaribari Chache kaunti ya Kisii, mwenyekiti wa Maktaba nchini Samuel Nyangezo aliomba wanasiasa na viongonzi walio mamlakani kuweka kando tabia ya kuwakabidhi vijana pesa.  

“Hizi pesa mnawakabidhi vijana haziwasaidii kamwe. Kama munahitaji kujiimarisha kisiasa pesa hizo naomba mzikusanye pamoja ili zitumike kuanzisha academia ya michezo ili vijana hao waweze kuinua vipaji vyao kama vile kucheza mpira, kukimbia na michezo ya aina mbalimbali. Pesa hizi mnazowapa vijana haziwezi kuinua jamii ya Kisii kamwe,” alisema  Nyangezo.

Aidha, mwenyekiti huyo aliomba viongonzi walio katika mamlaka kujiunga pamoja kama viongonzi wa Kisii kufanya maendeleo pamoja badala ya kutofautiana kisiasa.

“Naomba viongonzi wa Kisii mfanye maendeleo. Hizi siasa za mdomo haziwezi kusaidia mwananchi wa kawaida. Wakati wa siasa utafika lakini kwa sasa ni maendeleo mnastahili kuleta ili eneo letu la Kisii liinuke zaidi kimaendeleo,” aliongeza Nyangezo.