Mwanamme akiwa katika shamba la unyunyizaji la Galana-Kulalu

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Viongozi kutoka kaunti ya Kilifi wameapa kuwa hawataruhusu mradi wa unyunyizaji mashamba wa Galana- Kulalu kupewa mtu wa kibinafsi jinsi inavyopendekeza serikali kuu.

Viongozi hao wanasema kuwa serikali ina mpango wa kunyakua shamba hilo jambo ambalo wamesema kuwa hawataruhusu lifanyike.

Akizungumza eneo la Matsangoni siku ya Jumatano, Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya alisema kuwa Serikali kuu imeshindwa kuendeleza mradi huo na sasa inataka kutumia njama fiche kunyakua Mashamba ya wakaazi. 

Hatua hii inakujia baada ya wizara ya maji    siku ya Jumatano wiki iliyopita kutangaza kuwa ina mpango wa kupeana ekari 20,000 ya Mashamba kwa mmiliki wa kibinafsi ili kuongeza uzalishaji wa zao la Mahindi.

‘‘Kama viongozi wa eneo hili hatutaruhusu jambo hilo kufanyika.K Kupeana mashamba yetu kwa mtu hatufahamu hatutaki na hatutakubali,’’ alisema Baya.

Waziri wa maji Eugene Wamalwa alisema kuwa hatua hiyo inanuia kuhakikisha kuwa mmiliki wa kibinafsi pamoja idara ya kilimo inapanda mahinfdi ya kutosha eneo hilo.

Baya alisema kuwa atawaongoza Wabunge wa eneo hilo kupeleka lalama zao katika bunge la kitaifa ili litatuliwe.

‘‘Sisi kama Wabunge kutoka eneo hili,tutapeleka swala bungeni Nairobi katika kamati inayoshughulikia kilimo,’’ Baya aliongezea

Baya aliongezea kuwa watashinikiza wenyeji hadi mpango wa serikali kuu ufeli.