Baadhi ya viongozi katika jimbo la Nakuru wametoa lalama zao kutokana na kile wanachokitaja kama serikali kutotimiza kikamilifu malipo kwa wakongwe wa kuanzia miaka 65.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakiongea mjini Nakuru Jumanne wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la wazee katika eneo la bonde la ufa Gilbert Kabage viongozi hao, wamesema kuwa ni haki ya wazee hao kupata pesa walizo ahidiwa na serikali ambayo ni shilingi 2,000 kila mwisho wa mwezi.

“Wengi wetu wamekufa kutokana na ufukara na tulio hai tunaendelea kuishi maisha ya uchochole jambo ambalo halifai kwa wakongwe kama sisi ambao wengi wetu tulipigania uhuru wa nchi hii,” alisema Bw Kabage.

Baada ya mwanahabari huyu kuchunguza madai haya imebainika kuwa ni wengi ambao hawanufaiki kutokana na pesa hizi haswa kutoka maeneo ya Bahati, Njoro, Subukia na Gilgil .

Hata hivyo shutma hizo zimewalalia machifu na manaibu wao ambao wanadaiwa kutumia fursa hiyo kuandikisha watu ambao hawastahili kupokea fedha hizo.