Viongozi mbalimbali wa kisiasa katika Kaunti ya Nakuru walikusanyika siku ya Jumanne katika boma la marehemu Jane Gathogo kufariji familia yake.
Katika risala zake za rambirambi zilizosomwa na mkuu wa Idara ya Biashara katika Kaunti ya Nakuru Bi Anne Njenga, Gavana Kinuthia Mbugua alimtaja marehemu kama kiongozi aliyejitolea katika kuunganisha Wakenya.
Ni matamshi yaliyoungwa mkono na mwakilishi mteule Rosemary Okemwa ambaye alisema kuwa amempoteza rafiki wa karibu.
"Marehemu Jane alikuwa msaidizi na mshauri wangu wa kisiasa," alisema Okemwa.
Mshirikishi wa serikali ya Kaunti ya Nakuru Bi Zipporah Kimani kwenye hotuba yake alisema kuwa Kaunti ya Nakuru imepoteza kiongozi shupavu.
Matamshi sawia yalitolewa na mwenyekiti wa ‘Grassroot Women Empowerment’ Bi Grace Kibuku aliyesema kuwa wamempoteza kiongozi mpenda aman.
Mwanasiasa Ezekiel Kamau kutoka Mau Narok kwa upande wake aliwataka akina mama kuiga mfano wa marehemu Gathogo.
"Ombi langu kwa akina mama ni kwamba tuige mfano wa Jane Gathogo," alisema Kamau.