Viongozi wa kisiasa mjini Nakuru wamesema wako tayari kuandaa maombi ya kutoa shukrani kwa mwenyezi mungu kufuatia kuachiliwa huru kwa naibu rais William ruto na mwanahabari Joshua Arap Sang.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha jubilee Abdul Noor, viongozi hao wamesema kuwa itakuwa heshima kubwa kwa mji wa Nakuru kuandaa maombi hayo.

Noor amesema kuwa watu wa Nakuru wanampenda naibu rais na wako tayari kumkaribisha tarehe 16 mwezi huu, siku ambayo maombi hayo yataandaliwa.

“Ni heshima kubwa kwa mji wa Nakuru kuteuliwa kuweza kuandaa hafala hiyo maalumu ya kutoa maombi ya shukrani kwa mwenyezi mungu, na sisi kama wenyeji tuko tayari kuweza kumpokea naibu rais na kumwonyesha kuwa tumesimama pamoja na yeye,” alisema Noor.

Aidha, viongozi hao wametoa wito kwa wakazi wa Nakuru kujitokeza kwa wingi na kuhudhuria maombi hayo.